Mbunge Wa Embakasi Mashariki Babu Owino Aikosoa Serikali Kuhusu Mpango wa Ebola

Kauli yake inajiri huku mjadala ukiendelea nchini kuhusu mpango wa kuanzisha kituo cha karantini na maandalizi ya kukabiliana na Ebola

R

Rware Media Services

2 Jun 2026

8 days ago

Filed Under

MP Embakasi East Babu Owino

Share this article

Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, ameikosoa serikali kuhusu kile alichodai kuwa ni manufaa madogo ambayo Kenya itanufaika nayo kupitia mpango unaohusishwa na maandalizi dhidi ya ugonjwa wa Ebola.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Babu alisema kuwa serikali imeeleza kuwa itapata takriban Sh1.7 bilioni kutokana na mpango huo. Kulingana naye, kiasi hicho kikigawanywa kwa Wakenya milioni 58, kila mmoja atapata takriban Sh29 pekee.

Mbunge huyo alihoji mantiki ya kukubali mpango huo kwa manufaa ambayo amedai ni madogo mno ikilinganishwa na hatari zinazodaiwa kuhusishwa nao.

“Nikigawanya Sh1.7 bilioni kwa Wakenya milioni 58, kila mtu atapata Sh29. Tunaletewa virusi vya Ebola juu ya shilingi 29. Hizo zinaweza kununua hata Panadol?” alihoji Babu.

Kauli yake inajiri huku mjadala ukiendelea nchini kuhusu mpango wa kuanzisha kituo cha karantini na maandalizi ya kukabiliana na Ebola katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Laikipia.

Hata hivyo, serikali imeendelea kusisitiza kuwa kituo hicho ni sehemu ya mkakati mpana wa taifa wa kujiandaa na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na kwamba hakina lengo lolote la kuhatarisha afya ya wananchi.

Mjadala huo umeibua maoni tofauti kutoka kwa viongozi wa kisiasa, wataalamu wa afya na wananchi kuhusu manufaa, uwazi na athari za mpango huo.

source attributed: Mpasho News